Staa wa muziki nchini Tanasha Donna amelazimika kuomba msamaha kwa kushindwa kulipa pesa za mtoa huduma wa masuala ya urembo aitwaye Zena Glam.
Kupitia ukurasa wake wa instagram tanasha amesema tayari ashamlipa mrembo huyo pesa zake huku akiomba radhi kwa kile kilichofanyika kwa kusema kwamba hahusiki moja kwa moja na masuala ya fedha kwani kuna timu ambayo inashughulika na pesa wakati wa kutayarisha video za nyimbo zake.
Pesa ambazo tanasha donna amekuwa akidaiwa imetokana na gharama ya shughuli ya kuandaa video ya wimbo wake wa Kalypso ambao ulifanyika mwezi novemba mwaka jana.
Kauli ya tanasha donna inakuja siku chache baada ya aliyekuwa mtangazaji wa runinga moja nchini dana de Grazia maarufu kaka hustle Goddess kudai kwamba msanii huyo amekataa kulipa deni la rafiki yake ambaye anajishughulisha na masuala ya urembo.
Baada ya deni hilo kulipwa Bi Grazia alitumia mitandao yake ya kijamii kuwataarifu watu kwamba tanasha amekalisha deni alilokuwa anadaiwa na rafiki yake na hatua kumwaanika msanii huyo haikuwa ya nia mbaya.