Staa wa muziki nchini Uganda Cindy Sanyu amesema kwamba hajutii kukosa kwenye orodha ya wasanii walioteuliwa kuwania tuzo za MTV MAMA Awards.
Kulinga na Cindy Sanyu kutotajwa kwake kwenye tuzo hizo haitabadilisha chochote kwenye maisha yake ikizingatiwa kuwa tayari ana mafanikio makubwa kwenye muziki wake.
Kauli ya cindy inakuja mara baada ya wadau wa muziki nchini Uganda kudai kwamba msanii huyo alikasirika baada ya jina lake kukosa kwenye orodha ya wasanii waliotajwa kuwania tuzo za MTV MAMA.
Ikumbukwe Cindy alikuwa amependekeza tuzo za MTV MAMA ziahirishwe kwa kigezo kuwa Waganda wana masuala mengi neambayo yamewaathiri kutokana na janga la Corona huku akipinga hatua ya waandaji wa tuzo hizo kumleta DJ Khaled kutoka nchini Marekani awe mshereheshaji wa tuzo hizo.