Nyota wa muziki nchini Nadia Mukami ameibua mjadala mzito kwenye mtandao wa Twitter mara baada ya kudai kwamba yeye ndiye mwandishi bora wa nyimbo wa kizazi chake.
Kupitia misururu ya tweets kwenye ukurasa wake wa Twitter mkali huyo wa Ngoma ya “Kolo” amependekeza kuwepo kwa tuzo za mwandishi bora wa mwaka nchini huku akidai kwamba pana haja ya wadau wa muziki nchini kuelekeza mawazo yote kwenye suala la uandishi wa nyimbo.
Haikushia hapo mrembo huyo alienda mbali zaidi na kusema kwamba amefurahia kuibua mjadala kuhusu uandishi wa nyimbo kwenye kiwanda cha muziki nchini kwani ni suala mtambuka ambalo linapaswa kuangaliwa kwa jicho la tatu.
Kufuatia kauli hiyo ya Nadia Mukami kuhusu suala la uandishi wa nyimbo imeibua hisia mseto miongoni mwa wakenya kwenye mtandao wa Twitter ambapo baadhi wameonekana kuunga mkono madai ya msanii huyo huku wengine wakitofautiana nae wakidai kwamba wao sio mashabiki wa muziki wake.