Mapema mwaka wa 2020 bosi wa lebo ya muziki ya Gagamel, Bebe Cool alimuonya msanii King Saha aache kutumia mihadarati kwa sababu inaathiri shughuli za kimuziki ya msanii huyo.
Sasa hatua hiyo haikupokelewa na baadhi ya wadau wa muziki nchini Uganda ambao walienda mbali na kumshambulia King Saha bila uoga huku wakimtaka msanii akome kutumia dawa za kulevya.
Mwaka mmoja sasa umepita na King Saha inaoneka hajeacha matumizi ya mihadarati kwani aliyekuwa mpenzi wake Joweriah Ali ameoneshwa kusikitishwa na namna msanii huyo anaendelea kutumia mihadarati.
Kupitia mitandao yake ya kijamii amewataka wasanii wa muziki nchini Uganda kuungana na kumpeleka msanii huyo kwenye kituo cha matibabu ya watumiaji wa pombe na mihadarati kabla ya umauti kumkuta.