Akaunti ya Instagram ya Sanaipei Tande yenye followers laki imedukuliwa (hacked) Jumatano wiki hii.
Tayari hacker huyo ameibadilisha jina la akaunti ya msanii huyo na kuipa jina la ‘Instagram Support’ huku akifuta picha zake zote alizoziweka mwaka huu.
Sanaipei Tande anakuwa msanii wa hivi karibuni ambaye akaunti yake ya Instagram imedukuliwa.Miezi kadhaa iliyopita akaunti ya msanii Kelechi Africana pia ilidukuliwa japo alifanikiwa kuirejesha.
Ikumbukwe miaka ya hivi karibuni akaunti za mastaa wa muziki nchini zimekuwa moja ya vyanzo vyao muhimu vya kipato na wale wenye followers wengi wamekuwa wakipata deals zenye hela nyingi.