Kiongozi wa chama cha National Unity Platform (NUP) Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, ameagiza mawakili wake kuondoa mahakamani kesi ya kupinga ushindi wa rais Yoweri Kaguta Museveni, uchaguzi alikuwa akiupinga baada ya matokeo ya uchaguzi huo Januari 14 mwaka huu.
Bobi Wine amesema wameondoa kesi hiyo kwa msingi ya baadhi ya majaji kuegemea upande moja wa kesi, na kuongeza kuwa hapangi kuzua vurugu baada ya kundoa keshi hiyo katika mahakama ya Owiny Dollo.
Hatua yake inajiri siku moja tu, baada ya rais Museveni, tume ya uchaguzi na mwanasheria mkuu, kutoa hati kiapo kwa mahakama, ili kujibu tetesi 53, za upande wa mashtaka kuwa uchaguzi wa Januari 14 haukuwa wa huru na haki.
Mkurugezi wa maswala ya sheria katika chama tawala NRM, Oscar Kihika, amewaambia wanahabari jijini Kampala kuwa Bobi Wine atalazimika kugharimia gharama zote za kesi hiyo hasa baada ya kujiondoa.