BENKI EQUITY KUTOA SHILLINGI BILLIONI 75 KWA WAKULIMA WADOGO WADOGO NCHINI

You are currently viewing BENKI EQUITY KUTOA SHILLINGI BILLIONI 75 KWA WAKULIMA WADOGO WADOGO NCHINI
  • Post category:Biashara

Benki ya Equity inapanga kutoa shilingi billioni 75 kwenda kwa wakulima wadogo wadogo.

Kulingana na afisa mtendaji wa benki hiyo, James Mwangi, benki ya Equity imeshirikiana na washikadau wengine wa kutoa mikopo ili kuwasaidia wakulima kupata fedha hizo kwa riba ya chini kwa miaka mitano.

Mwaka uliopita serikali ya Kenya iliweka wazi kutoa shilingi billioni 10 kwenda kwa wafanyibiashara wadogo wadogo  kama njia moja ya kuwakwamua kutoka kwa makali ya COVID-19.

Kadhalika Mwangi anasema kwamba ushirikiano wao na wakfu wa Mastercard uliwawezesha kutumia shilingi milloni 100 kwenda kwa wafanyibiashara huku ile ya Propaco ikitoa shilingi millioni 100.

Mwangi alisema haya baada ya kuzindua mradi wa miaka 7 wa shilingi billioni 16.7 kutoka kwa Benki ya Ulaya iliyo na riba ya chini.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa