Wakulima bonde la ufa wameelezea wasiwasi wao kutokana na deni la Shilingi bilioni kumi na sita zinazodaiwa bodi ya mazao na nafaka nchini NCPB na benki ya KCB ambalo limepelekea kusitishwa malipo ya ununuzi wa mahindi kwa Shilingi alfu mbili mia saba.
Mwenyekiti wa wakulima kaskazini mwa bonde la ufa Kipkorir Menjo anasema hali hii imezua wasiwasi miongoni mwa wakulima ambao kwa sasa wamedinda kuwasilisha mahindi yao katika bodi hiyo wakihofia kukosa malipo.