Mgombea urais wa klabu ya Barcelona, Joan Laporta ameijia juu timu ya PSG wanaomuwania mchezaji wao nyota Lionel Messi kwa kuwaambia kuwa wanapuuzia kanuni za matumizi ya fedha katika usajili.
Kwa mujibu wa Mtandao wa Goal, Laporta ametoa kauli hiyo baada ya Klabu hiyo kuongoza katika mbio za kumuwania nyota huyo atakayemaliza mkataba wake na timu hiyo mwezi Juni mwaka huu.
Laporta anawalaumu PSG kwa kukosa heshima baada ya timu hiyo kutoa kauli hivi karibuni kuwa Messi atakuwa katika rada zao kila wakati na ni lazima atue katika klabu hiyo.