Baada ya maswali kuwa mengi kuhusiana na muhusika wa ujauzito wake,hatimaye msanii wa Bongo fleva Amber Lulu amemtaja msanii kutoka kundi la “B.O.B Micharazo ” Emba Botion kuwa ndiye muhusika wa ujauzito wake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Amber Lulu amepost picha ya Mr Botion na kuandika “Naona maswali yenu yaishie hapa baba K uyo apoo, Sito kuwepo insta kwa muda Kidogo”
Ikumbukwe kabla ya Amber Lulu kumtambulisha baba wa mtoto wake huyo watu wengi walihisi kwamba Prodyuza P-Funk Majani ndio mhusika wa ujauzito wake taarifa ambazo mrembo huyo alikuja akazikana kwa kudai kwamba hajawahi kutoka kimapenzi na P-Funk Majani kama inavyosemwa mitandaoni.