Mama mzazi wa Msanii wa Gengetone anayefanya vizuri nchini Trio Mio, Irma Sakwa amemuanika tapeli mashuhuri aitwaye Wilkings Fadhili kwa madai ya kumtapeli msaani huyo zaidi ya shillingi laki moja.
Katika taarifa, Mama Trio Mio (Irma Sakwa) ametangaza kwamba Fadhili hatakuwa tena meneja wa mtoto wake na hivyo haruhusiwi kufanya biashara yoyote kwa niaba yake.
“Wilkings Fadhili sio tena meneja wa Trio Mios. Jamaa huyu amebobea kwenye sanaa ya utapeli. Huyu jamaa amemtapeli mwanangu zaidi ya 100k. Jihadharini! Haruhusiwi kufanya biashara yoyote kwa niaba ya mwanangu Trio Mio, ” Mama Trio Mio alichapisha kwenye mtandao wake wa kijamii.
Wakati huo huo, Fadhili pia ameshtumiwa na mchungaji Suzie Wokabi kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, ambaye amedai kwamba jamaa huyo alitoweka na video zake, jambo ambalo lilimlazimu kutofanya kazi na Fadhili ambaye alikuwa msimamizi wa podcast yake.
Ikumbukwe Wilkings Fadhili sio mgeni kuzushiwa tuhuma kama hizo, mwaka wa 2019, mwandishi wa BBC Larry Madowo alitishia kumshtaki baada ya kugundua kuwa jamaa huyo alikuwa akitumia jina lake kuwatapeli Wakenya.