Mkongwe wa muziki wa Raggae kutoka nchini Jamaica Bunny Wailer amefariki dunia siku ya jana “March 02, mwaka 2021 akiwa na umri wa miaka 73.
Kifo chake kimethibitishwa na meneja wake Maxine Stowe na afisa utamaduni wa Jamaica “Olivia Grange”.
Sababu ya kifo cha mkongwe huyo haijawekwa wazi moja kwa moja lakini tangu mwezi Julai mwaka 2020 alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi ambao ulimpelekea kulazwa hospital mara kwa mara.
Bunny Wailer alikuwa ni mmoja kati ya wanachama na waanzilishi wa kundi la “The Wailers” ambalo alikuwa na wasanii wengine akiwemo marehemu Bob Marley, Peter Tosh na Marcia Griffiths.