Album ya Darassa “Slave Becomes A King” inaendelea kufanya makubwa kwenye mitandao ya kuuza na kusikiliza muziki duniani.
Mpaka sasa imefikisha jumla ya streams MILIONI 138 kwenye majukwaa yote ya kusikiliza na kupakua muziki duniani.
Album hiyo ya “Slave Becomes A King” iliachiwa rasmi Disemba 24, mwaka wa 2020 ikiwa na jumla ya mizinga 21.
Hadi sasa darassa ameachia video mbili kutoka kwenye album hiyo ambazo ni Proud Of You na Waiter ukiacha ‘I Like It’ aliyomshirikisha Sho Madjozi ambayo ilitangulia.