DR. DRE AREJEA KAZINI BAADA YA KUUGUA NA KULAZWA “ICU”.

You are currently viewing DR. DRE AREJEA KAZINI BAADA YA KUUGUA NA KULAZWA “ICU”.
  • Post category:Burudani

Baada ya kutoka hospitalini mtayarishaji wa muziki nchini Marekani, Dr. Dre amerejea studio huku ikiaminika kuwa huenda akaendeleza mpango wake wa awali wa kuandaa albamu yake kwa jina, “Detox”.

Dr. Dre aliyelazwa katika hospitali ya Cedars-Sinai mjini Los Angeles kutokana na tatizo la kuvilia damu kwenye ubongo baada ya mshipa kuvimba na kupasuka.

Dre aliruhusiwa kutoka hospitali Januari 15 na kesho yake, Dem Jointz ambaye ni mmoja wa watayarishaji wake wa muziki aliweka picha ikionyesha Dr. Dre na wengine ndani ya studio akisema wamerejea.

Kwenye maelezo ya picha hiyo, Dem Joints aliongeza maneno”Detox21″ kuashiria kwamba Dre na watayarishaji wake wa muziki watarejelea kwenye kazi ya Dre ya mwaka 2015 kwa jina “Detox”.Mpaka sasa Dr.

Hata hivyo Dre hajasema chochote kuhusu picha hiyo iliyopostiwa na Dem Jointz, na Pia Dre hajathibitisha juu ya maendeleo ya albamu yake ya Detox.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa