NITAENDELEA NA MUZIKI LICHA YA KUSHINDA UBUNGE-ASEMA DKT. HILDERMAN.

You are currently viewing NITAENDELEA NA MUZIKI LICHA YA KUSHINDA UBUNGE-ASEMA DKT. HILDERMAN.
  • Post category:Burudani

Mwanamuziki kutoka Uganda Dakta. Hilderman ambaye juzi kati aliteuliwa kama Mbunge wa eneo la Mawokota amedokeza kuwa hana mpango kuacha biashara ya muziki.

Hilderman ametujuza hayo kwenye moja ya interview ambapo amesema ataendelea kufanya muziki wake kama kawaida lakini pia atatumbuiza kwenye matamasha mbali mbali ya muziki.

Aidha amedokeza kuwa ana mpango wa kumtambulisha msanii mwingine kutoka eneo Mawokota ambaye atachukua nafasi yake kwenye tasnia ya muziki nchini  Uganda.

Hata hivyo, Hilderman amesema hataonekana kwenye matamasha ya muziki mara kwa mara kama ilivyokuwa miaka ya hapo nyuma kwa sababu atakuwa ameshikika na kazi ya kuwatumikia wananchi wa Mawokota huku akitujuza pia ana mpango wa kuhudumu kama mbunge kwa vipindi viwili.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa