WAZIRI WA AFYA KAUNTI YA EGEYO MARAKWET KIPRONO CHEPKOK ASIMAMISHWA KAZI KUTOKANA NA UTENDAKAZI DUNI

Gavana wa kaunti ya Elgeiyo Marakwet mhandisi Alex Tolgos amesimamishwa kazi kwa muda Waziri wa Afya kaunti hiyo Kiprono Chepkok kufuatia lalama za wananchi na utendakazi mbaya ofisini.

Akizungumza na wanahabari mjini Iten gavana Tolgos ametoa onyo kali kwa maafisa wote wa serikali watakaozembea kazini kuwa watawachukulia hatua kali za kisheria kwa kupokonywa nyadhifa zao.

Aidha Tolgos amesema ni wajibu wake kwa sasa kuhakikisha wakaazi wa kaunti hiyo wanahudumiwa ipasavyo wakati huu ambapo anakamilisha hatamu yake ya uongozi.

Hata hivyo amemteua waziri wa fedha kaunti ya Elgeyo Marakwet Isaac Kamar kushikilia nafasi hiyo japo kikaimu huku akisistiza kuwa wizara ya afya inaendeleza mikakati ya kukabili maambukizi ya virusi vya Corona.

Robert Elim

Presenter and News Editor at North Rift Radio Kenya