Akina mama wametakiwa kuhakikisha watoto wanapata lishe bora ili kuwawezesha kukua na kuimarika kiafya.
Mtaalamu wa maswala ya lishe bora katika Hospitali ya Rufaa ya Kapenguria Jane Limang’ura anasema mtoto anafaa kunyonyeshwa kwa kipindi cha miezi sita kabla ya kupewa vyakula vingine vyenye madini
Aidha Limang’ura amewataka akina mama kutembelea vituo vya afya wanapokuwa wajawazito ili kuelimishwa kuhusiana na mbinu za kuhimarisha lishe kwa manufaa ya wanao.