WAKAAZI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WASHAURIWA KUFWATA MAELEZO YA SERIKALI.

You are currently viewing WAKAAZI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WASHAURIWA KUFWATA MAELEZO YA SERIKALI.

Wamiliki wa hoteli, vyumba vya burudani, maduka ya jumla pamoja na wahudumu wa magari ya uchukuzi wa umma Gatuzi la Pokot Magharibi wametakiwa kufwata vigezo vyote vya Serikali mara moja.

Idara ya Usalama Gatuzi hilo limesema ni sharti baa zote zifungwe kama alivyoagiza Waziri wa Afya Mutahi Kagwe huku magari ya uchukuzi wa umma ukitakiwa kuzingatia maelezo ya Serikali ikiwemo kupunguza abiria wanaoabiri magari hayo pamoja na kuzingatia usafi wa hali ya juu,

Aidha idara hiyo imewataka wananchi kuzingatia umbali wa mita moja huku wakishauriwa kusalia katika makaazi yao ili kuzuia kuenea kwa Virusi hivyo hatari huku ikisema watakaokaidi masharti ya Serikali watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.