WANAKANDARASI KAUNTI YA POKOT WATAKIWA KUKAMILISHA MIRADI YA MAENDELEO KWA WAKATI

You are currently viewing WANAKANDARASI KAUNTI YA POKOT WATAKIWA KUKAMILISHA MIRADI YA MAENDELEO KWA WAKATI

Kamishna wa Kaunti ya Pokot Magharibi Apollo Okello anasema afisi yake itaendelea kushinikiza utekelezaji wa miradi ya serikali kaunti hiyo ili kufanikisha ajenda nne kuu za utawala wa rais Uhuru Kenyatta.

Okello ametoa wito kwa wanakandarasi kuhakikisha kwamba miradi ya serikali inakamilishwa bila kuhusisha visa vya ufisadi.

Aidha amewahakikisha wananchi kwamba miradi yote iliyoanzishwa na serikali ya kitaifa itakamilishwa kwa wakati na kuwafaidi wananchi.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.