Wakulima katika kaunti ya Uasin Gishu wametakiwa kukumbatia mbinu za kisasa za ufugaji kama njia mojawapo ya kuboresha uzalishaji
Akizungumza katika kituo cha kilimo cha Chebororwa Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jackson Mandago anasema kuna manufaa mengi kwa wakulima kukumbatia kilimo cha kisiasa kwani wataongeza mapato na kujiinua kiuchumi
Aidha baadhi ya wakulima wamekiri kuwapo na bei duni kwa mifugo wao huku wakiahidi kukumbatia mbinu za kisasa ili kupata bei nzuri kwenye soko ya sasa yenye ushindani mkubwa