WAKENYA WALALAMIKIA GHARAMA YA JUU YA MAISHA.

You are currently viewing WAKENYA WALALAMIKIA GHARAMA YA JUU YA MAISHA.
  • Post category:Biashara

Tangu kurejeshwa kwa ushuru unaotozwa bidhaa baada ya kulegezwa vizuizi vya kuzuia virusi vya corona, mkenya wa kawaida wa kipato cha chini ameanza kuhisi uzito wa gurudumu la maisha ambalo lilikuwa hata nzito zaidi wakati wa kipindi kigumu na kirefu cha tandavu ya covid-19

Katika tathimini yetu kwenye biashara ndogo ndogo na kati mjini Kapenguria na mjini Kitale Kaunti ya Pokot Magharibi na Trans-nzoia mtawalia idadi ya wateja au wanunuzi ni haba nao wafanyibiashara wanashiriki gumzo, pilkapilka za awali hazipo kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha yaani hamna wanunuzi.

Katika soko la Makutano ambalo huwa na shuguli na watu wengi, wanaunuzi wanahesabika tu, tunakutana na mama mmoja ambaye ni mfanyibiashara mkongwe amekuwa katika soko hili kwa miaka 25 na zaidi ananielezea namna biashara yake ya kuuza viazi mbatata, mboga na matunda ilivyoadhirika kutokana na uhaba wa wanunuzi.

Si yeye tu kushoto kwake yuko mfanyibiashara mwingine kwa jina Ann Cheyech ambaye ananielezea namna hali ilivyo sasa kibiashara ikilinganishwa na  kitambo hususan kuhusu biashara yake ya hoteli.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.