KENYA KUJENGA KIWANDA CHA KUZALISHA MBOLEA CHA TAKRIBAN SHILLINGI BILLIONI 3.

You are currently viewing KENYA KUJENGA KIWANDA CHA KUZALISHA MBOLEA CHA TAKRIBAN SHILLINGI  BILLIONI 3.
  • Post category:Biashara

Kenya inatarajiwa kujenga kiwanda cha kuzalisha mbolea kitakachogharimu takriban shilingi billioni 3.

Kiwanda hicho kwa jina Fertiplant East Africa Limited kinatarajiwa kujengwa mjini Nakuru mwezi ujao ambapo kitazalisha takriban magunia millioni 2 kila  mwaka.

Hapo awali wasimamizi wa kiwanda hicho walidokeza kukifungua Disemba mwaka jana ila janga la Corona likachangia kusitishwa kwa shughuli hiyo.

Kumbuka kwamba ujenzi wa kiwanda hicho ulianza mnamo mwaka 2015 huku kikifadhiliwa na oikocredit pamoja na benki ya NCBA.

Kadhalika mkurungezi wa kiwanda hicho Titus Gitau anasema kwamba watazalisha mbolea ya kupanda majani chai, kahawa, viazi, mahindi na miwa.

Vile vile mbolea hiyo itauzwa kwenda kwa mataifa ya nje kama vile Uganda, Rwanda na Burundi na kufikia sasa Kenya hutumia takribani tani alfu mia tano kila mwaka.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa