VIONGOZI WA KISIASA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUSAMBAZA MASKI MASHINANI

Wakaazi Kaunti ya Pokot Magharibi wameshauriwa kuzidi kuzingatia masharti yaliyowekwa na wizara ya afya kuthibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Kwenye mazungumzo ya kipekee na idhaa hii, Mwakilishi wadi mteule Grace Rengei anasema kwamba huenda Wakenya wengi wakaathiirika kwenye wimbi la tatu la maambukizi ya corona ikiwa hawatatilia manani maelezo ya Wizara ya afya.

Aidha ametoa wito kwa uongozi wa Kaunti ya Pokot Magharibi sawa na viongozi wa kisiasa kuhakikisha kwamba wanasambaza maski kwa wananchi hasa mashinani ili kuwasetiri dhidi ya maambukizi.

Tamko la rengei linajiri siku chache baada ya Waziri wa afya kaunti ya pokot magharibi jack Yaralima kuwahimiza wananchi kuvalia barakoa kama njia moja ya kuzuia msambao wa virusi vya corona ikizingatiwa kwamba wimbi la tatu limeripotiwa nchini.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.