Vijana kutoka kaunti ya Elgeiyo Marakwet wakiongozwa na Dennis Cherono wamewakumbusha wenzao kwamba hakuna faida yoyote ambayo watapata kwa kuvuruga amani ingekuwa bora wajihusishe zaidi kwenye maswala ambayo yanaweza kuwafaidi
Kwenye mkao na waandishi wa habari mjini Eldoret, vijana hao wanaitaka serikali kuwasaidia vijana kwa kuliangazia swala la ukosefu wa ajira ambalo wanasema limewakumba vijana wengi nchini hali ambayo imechangia wengi wao kutumika vibaya.
Kuhusu mchakato wa BBI vijana hao wanataka kila mkenya apewe nafasi ya kutoa maoni yake bila kuwa na vizuizi na mapendeleo yeyote ili iwe na manufaa kwao baada ya kura ya maamuzi kufanyika.