Serikali ya kaunti ya Pokot Magharibi imeipongeza wizara ya afya nchini pamoja na wahudumu wa afya kwa kusambaza chanjo dhidi ya Corona.
Gavana wa kaunti hiyo John Lonyangapuo,anasema kuwa serikali yake iko tayari kwa chanjo ya Corona inayosubiriwa kuwasili hapo kesho,akisema watu ambao watakuwa mstari wa mbele kuwahudumia wananchi watapewa kipau mbele.
Aidha anasema viongozi wamewapa kipau mbele wananchi katika chanjo hiyo huku akisema hawapaswi kuwa na hofu kwani tayari utafiti wa kutosha umefanywa.
wakati huo huo amewasihi Wakenya kuendelea kuzingatia kanuni na sheria zilizowekwa kuthibiti msambao wa Corona.