Maandamano yameendelea kwa siku ya pili Nchini humo baada ya mvutano kati ya Wafuasi wa Kiongozi wa Upinzani, Ousmane Sonko na Polisi kufuatia shutuma za ubakaji ambazo Mwanasiasa huyo anazikataa
Sonko ambaye alikuwa nafasi ya tatu katika Uchaguzi Mkuu 2019 anashikiliwa na anatarajiwa kuhojiwa baada ya kinga ya Bunge aliyokuwa nayo kuondolewa wiki iliyopita
Serikali imethibitisha kifo kimoja kufuatia ghasia hizo na Mamlaka zimelitaka Jeshi kusaidia Polisi kukabiliana na maandamano ambayo huenda yakaendelea zaidi