Siku moja tu baada Mbunge wa Soy kutimuliwa katika nafasi ya Naibu Katibu mkuu wa chama cha Jubilee, mbunge wa Cherang’any katika kaunti ya Trans-Nzoia, Joshua Kutuny ambaye amechukuwa nafasi hiyo amesema atatumia kuimarisha demokrasia chamani.
Akihutubu katika shule ya upili ya Nyakinywa, ametaja uteuzi huo kuwa heshima kwa wananchi wa Cherangani na kuongeza kuwa wakenya wanashabikia amani na umoja wa taifa.
Aidha amesema atatumia fursa hiyo kuipigia debe mswada wa 2020 wa marakebisho ya katiba kupitia mpango wa maridhiano ya kitaifa BBI akisema ina manufaa mengi kwa wananchi.