Walimu na wanafunzi katika eneo la Kapedo wamehakikishiwa usalama wao licha ya oparesheni inayoendelea kwa sasa.
Mshirikishi wa Bonde la Ufa George Natembea amewataka walimu sawa na wanafunzi kurejea shuleni juma lijalo akisema lengo la maafisa wa usalama wanaoendesha oparesheni ni kuwasaka wahalifu wanaotatiza amani eneo hilo.
Aidha Natembea amepuzilia mbali madai kwamba maafisa wa usalama wamekiuka haki za binadamu kwa kudhulumu raia akisisitiza kwamba hajapokea ripoti yoyote kuhusiana na hilo.