GAVANA WA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI AHUTUBIA WANANCHI BAADA YA LIKIZO YA SIKU 30

You are currently viewing GAVANA WA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI AHUTUBIA WANANCHI BAADA YA LIKIZO YA SIKU 30

Baada ya kutoweka kwa kipindi cha mwezi moja huku maswali mengi yakiulizwa na wakaazi wa Pokot Magharibi waliotaka kujua alipo Gavana wao, hatimaye gavana John Krop Lonyangapuo alijitokeza akindamana na wandani wake Mbunge wa Pokot Kusini David Pkosing, Mjumbe wa Sigor Peter Lochakapong, Mbunge wa Kacheliba Mark Lomnokol na Mwakilishi wa akina Mama Lilian Tomitom.

Lonyangapuo alingia Mjini Makutano kwa mbwembwe na ucheshi Wake ambao Wanachi walikua wameukosa kwa muda.

Gavana Lonyangapuo alitumia fursa hio kuwaeleza Wakaazi wa Pokot Magharibi kwamba alikua kwenye likizo ya mwezi mmoja huku akiwasuta baadhi ya Viongozi Kaunti hii waliokua wakieneza propaganda kwamba wanapaswa kuheshimiana.

Aidha amewataka viongozi kaunti hii kuombeana mema licha ya kuepo na utofauti wa kisiasa.

Viongozi walioandamana na Gavana Lonyangapuo walitumia  nafasi hio kuitaka Serikali kuu kutotumia nguvu wanapoendesha oparesheni ya kuwasaka Wahalifu katika eneo la Kapedo Kaunti ya Baringo, Mbunge wa Kacheliba Mark Lomnokol akisema Serikali kuu inapaswa kulaumiwa kwa kuzembea kazini.

Lomnokol ameitaka Serikali kuwapa muda Viongozi kutoka Jamii mbili zinazohasimiana kuketi chini na kufanya mazungumzo badala ya kutumia nguvu akisema hatua hiyo itazidisha uhasama hata zaidi.

Kauli hiyo imetiliwa mkazo na Gavana wa Pokot Magharibi John Lonyangapuo anayesema matatizo inayokumba Jamii ya Pokot ni sawa na ile ya Turkana akitaka mazungumzo ya haraka kufanywa baina ya Viongozi kutoka Jamii hizo mbili ili kutatua mzozo uliopo.

Ikumbukwe katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na maswali mengi kuliko majibu kutoka kwa Wananchi wa Kaunti ya Pokot Magharibi haswa wanaompinga na wanaomunga mkono Gavana Lonyangapuo wakitaka kujua alipo na hatimaye jibu limepatikana baada ya Gavana kujitokeza.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.