WACHUUZI WA MIFUGO KATIKA SOKO LA LODWAR WAFANYA UCHAGUZI WA KUTEUA VIONGOZI WAO.

You are currently viewing WACHUUZI WA MIFUGO KATIKA SOKO LA LODWAR WAFANYA UCHAGUZI WA KUTEUA VIONGOZI WAO.

Wachuuzi wa mifugo kaunti ndogo ya turkana ya kati wamewachagua viongozi watakaowasimamia kwenye shughuli zao za kibiashara katika soko kuu la miifugo la lodwar katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Kwenye uchaguzi huo ulioendeshwaa na tume uhuru  ya uchaguzi n  mipaka nchini IEBC, Lucas Kaaman amechaguliwa kama mwenyekiti wa soko la mifugo la lodwar akisaidiwa na Eyanae Lopuskidiama huku Lorogoi Eyane akichaguliwa kama katibu wa soko hilo akisaidiwa na Christopher Ekuam.

Akizungumza na wanahabari mjini baada ya kutangazwa mshindi Mwenyekiti mteule wa soko la mifugo la Lodwar James Kaaman amesema watahakikisha biashara ya mifugo katika soko la lodwar linahimarika ikizingatiwa kwamba ana mpango wa kutoa mikopo kwa wachuuzi lakini pia kuboresha mazingira ambayo wanaendesha shughuli zao za kibiashara.

Kwa upande wake katibu mteule wa soko hilo Lorogoi Eyanae amesema atahakikisha usalama unahimarishwa katika soko la mifugo la Lodwar huku akisisitiza  kwamba watakaopatikana wakishiriki  visa vya uhalifu katika soko hilo watakabiliwa kwa mujibu wa sheria.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Baraza la mauzo ya mifugo kaunti ya Turkana Joseph Losuru amesema uchaguzi huo umekuwa uhuru na wa haki huku akisema kwamba watahakikisha suala la usawa wa kinjisia unazingatiwa katika usimamizi wa Kamati ya wachuuzi wa soko la mifugo la Lodwar ikizingatiwa kuwa viongozi  waliochaguliwa ni wanaume pekee yao.

Hata hivyo Afisa mkuu katika idara ya uzalishaji wa mifugo katika kaunti ya Turkana Bob Ewoi amewataka viongozi waliochagulia kusimamia wa chuuzi katika soko la mifugo la Lodwar kutekeleza majukumu yao kikamilifu ili kuinua uchumi wa kaunti kupitia biashara ya mifugo huku akidokeza kwamba idara ya mifugo ina mpango kutoa mafunzo kwa wachuuzi wa mifugo kaunti ya turkana jinsi ya kuendeleza shughuli zao za kibiashara.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa