FRED GUMO AIKOSOA TUME YA NCIC KWA KUSHINDWA NA MAJUKUMU YAKE.

Siku chache baada ya Tume ya Maridhiano na Utangamano nchini NCIC kutoa orodha ya viongozi wachochezi, baadhi ya viongozi Magharibi mwa Kenya wanazidi kuilimbikizia lawama Tume hiyo kwa kupanda kwa joto la kisiasa linalozidi kushuhudiwa nchini.

Kwenye mahojiano na Mwanahabari wetu Charles Kemosi, Mwanasiasi mkongwe kutoka eneo la Magharibi Fred Gumo ameitaka  NCIC kuwajibikia utovu wa nidhamu unaozidi kukithiri kwenye majukwaa ya siasa la sivyo ivunjiliwe mbali iwapo imeshindwa na majukumu yake.

Gumo ametumia fursa hiyo kuwataka wanasiasa kukoma kutoa semi za chuki na kueneza siasa za kuwagawanya wananchi akidai kwamba ndio uchochea vurugu na ghasia katika mikutano ya kisiasa.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa