BUNGE LA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI LATETEA UWAMUZI WAKE WA KUPASISHA MSWADA WA BBI

You are currently viewing BUNGE LA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI LATETEA UWAMUZI WAKE WA KUPASISHA MSWADA WA BBI

Mswada wa marekebisho ya Katiba wa mwaka wa 2020 hauna uhusiano wowote na siasa za urithi mwaka wa 2022.

Kiongozi wa wengi katika bunge la Kaunti ya Pokot Magharibi Thomas Ngolesya Amutangorok anayesema mswada wa BBI unalega tu kufanyia katiba marekebisho ili kumfaa mwananchi wa kawaida.

Anasema uchaguzi mkuu ujao wa mwaka wa 2022 kila mkenya atapata nafasi ya kumchagua kiongozi anayefaa kuongoza katika ngazi mbali mbali.

Aidha ametetea hatua ya bunge la Kaunti ya Pokot magharibi kupasisha mswada wa BBI akisema sheria na taratibu zilizowekwa zilifwatwa kikamilifu.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.