Serikali ya kaunti ya Turkana imepokea zaidi ya matanki 20 ya maji yenye ujazo wa lita 1500 kutoka kwa Mamlaka inayosimamia raslimali za maji ya Central Rift ili kupiga jeki mapambano dhidi ya virusi vya corona kaunti hiyo.
Akizungumza alipopokea matanki hayo, Waziri wa Maji kaunti ya Turkana Joseph Namwar amesema matanki hayo ya maji yatasambazwa na kuweka kwenye maeneo ya umma ili kuwasaidia wananchi kwenye zoezi la kunawa mikono kila mara kuzuia kuenea kwa virusi vya Covid-19.
Aidha Namwar amesema serikali ya kaunti ya Turkana inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kupambana na ugonjwa huo kaunti hiyo ikiwa ni pamoja na kusambaza maji na vitakasa mikono au sanitizers.
Hata hivyo amewashukuru wadau hao kutokaMamlaka inayosimamia raslimali za maji ya Central Rift kwa msaada wao huku akiwataka wakaazi wa kaunti ya Turkana waendelee kushirikiana na serikali ya kaunti katika hatua zinazochukuliwa kukabiliana na ugonjwa huo.