BAADHI YA VIONGOZI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WASHTUMU UVAMIZI ENEO LA KAPEDO KUFUATIA MAUAJI YA AFISA WA NGAZI YA JUU WA GSU

You are currently viewing BAADHI YA VIONGOZI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WASHTUMU UVAMIZI ENEO LA KAPEDO KUFUATIA MAUAJI YA AFISA WA NGAZI YA JUU WA GSU

Mwakilishi wa Wodi mteule Kaunti ya Pokot Magharib Elijah Kasheusheu amelaani na kushutumu utovu wa usalama unaoendelea kushuhudiwa katika eneo la Kapedo.

Kwenye mahojiano ya kipekee na Northrift Radio, Kasheusheu amesema Serikali inafaa  kuwakamata washukiwa waliotekeleza uovu huo  mara moja ili sheria ifuate mkondo.

Kasheusheu aidha anapinga oparesheni ambayo Serikali imeanzisha eneo hilo akisema kuwa huenda Raia wasio na hatia wakaumia kufuatia maafisa wa Polisi kutumia nguvu kupita kiasi.

Nao wakaazi Kaunti ya Pokot Magharibi wakiongozwa na Musa Chepareraka, Paul Kamama. julius Merikit wamekashifu kitendo hicho na kuilaumu Serikali kwa kuanzisha  oparesheni Kapedo badala ya kuwakamata washukiwa kwanza.

Kwa upande wake Stephen Kolimuk kiongozi wa amani Pokot Magharibi amehoji kuwa ni jukumu la  Serikali kuhakikisha kuwa inawalinda  wananchi wake ikizingatiwa kuwa mwananchi yeyote ana haki ya kuishi popote.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.