Rapa 50 Cent kutoka Marekani anataka kuingia ulingoni kuzichapa na Floyd Mayweather.
Kwenye mahojiano yake kupitia “The Morning Culture”, 50 Cent aliulizwa ni nani anataka kupigana naye kwenye pambano la masumbwi na hakusita kumtaja hasimu wake huyo wa muda mrefu.
Aidha ameenda mbali zaidi ns kusema hofu yake kubwa ipo kwenye suala la uzito kwani hajui kama uzito wake unaweza fanana na wa MayWeather.
Ikumbukwe 50 Cent aliwahi kuwa memba wa karibu na Mayweather na hata kuingia naye ulingoni siku ya pambano na Oscar De La Hoya lakini wawili hao walikuja kupishana kutokana na kutokubaliana kibiashara.