COVID-19: Former Man United midfielder Marouane Fellaini is infected with the virus

You are currently viewing COVID-19: Former Man United midfielder Marouane Fellaini is infected with the virus
  • Post category:Michezo

Alikuwa fiti kwa Shandong Luneng kwa kuwasaidia kupanda ngazi hadi nafasi ya tano katika msimu wake wa kwanza na kutingisha wavu mara 13.

Goal kwa sasa inaripoti kuwa kiungo huyo wa kati ni mchezaji wa kwanza wa klabu hiyo bingwa nchini China kupatwa na virusi hivyo hatari. Sogora huyo mwenye miaka 32, anadaiwa kuwasili Jinan kwa mazoezi mnamo Ijumaa, Machi 20, akitumia treni wakati aligundiliwa kuwa na COVID-19. Ligi hiyo ya China kama nyingine kote ulimwenguni kwa sasa imesimamishwa huku taifa hilo likikabiliana na janga hilo la kimataifa ambalo limeangamiza maelfu ya watu. Huku hali hiyo ikiendelea kuzorota, ulimwengu wa soka umeibuka kuwa ulioathiriwa sana huku wachezaji wengi wakiendelea kupatwa na virusi hivyo. Mnamo Jumamosi, Machi 21, rais wa zamani wa Real Madrid, Lorenzo Sanz alilemewa na coronavirus huku staa wa Juve, Paulo Dybala pia akiambukizwa ugonjwa huo.