Mkataba wa Lionel Messi na klabu ya Barcelona umevuja, unatajwa kuweka rekodi kwenye historia ya mpira. Mkataba huo unaeleza kwamba Messi atapokea kiasi cha dolla milioni 673.9 ambazo ni sawa na takriban shillingi millioni 74 za Kenya kwa misimu Minne kama kila kitu kitaenda sawa kama walivyokubaliana.
Gazeti la El Mundo la nchini Uhispania ndilo limechapisha mkataba huo ambao Messi alisaini mwaka 2017 na unatajwa kuwa mkataba mkubwa zaidi kuwahi kusainiwa na mwanamichezo.
Baada ya kutoka kwa taarifa hiyo jana Jumapili, leo Lionel Messi na Barcelona wameripotiwa kuchukua hatua za kisheria kwa yeyote aliyevujisha mkataba huo ndani ya klabu lakini pia gazeti la El Mundo.