ZUCHU AWEKA REKODI MPYA YOUTUBE.

You are currently viewing ZUCHU AWEKA REKODI MPYA YOUTUBE.
  • Post category:Burudani

Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, msanii Zuchu amefikisha watu milioni 100 waliotazama kazi zake mbalimbali katika mtandao wa youtube kupitia channel yake rasmi.

Nyota huyo ambaye jina lake halisi ni zuhura, alijiunga na mtandao huo januari 29, mwaka wa 2019 na amepata watazamaji wengi kutokana na kazi zake mbalimbali anazoziweka katika mtandao huo. 

Hivyo zuchu anakuwa msanii wa kwanza wa kike Afrika Mashariki kufikisha watazamaji 100 millioni kwenye mtandao wa youtube.

Baadhi ya matukio anayoyaweka katika mtandao huo ni shoo anazozifanya, matangazo ya bidhaa na huduma, matukio makubwa anayoshiriki pamoja na utayarishaji wa video za nyimbo zake.

Tangu alipoanza kutoa kazi zake rasmi, miezi 9 iliyopita, Zuchu ameshaachia nyimbo mbalimbali ikiwemo Sukari, Nobody, na nyingine kibao.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa