WIZARA YA ELIMU YATAKIWA KUSHUGHULIKIA TATIZO LA UHABA WA WALIMU TURKANA

Wizara ya elimu imetakiwa kuajiri walimu zaidi katika kaunti ya Turkana kwani walimu waliopo hawatoshi kutoa huduma inayostahili kwa idadi kubwa ya wanfunzi iliyopo kwa sasa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu Ekwee Ethuro amesema juhudi zinazowekwa na serikali kuboresha sekta ya elimu ni bure iwapo tatizo la uhaba wa walimu litakosa kupata suluhu la kudumu.
Aidha Ethuro ametoa changamoto kwa serikali ya kaunti ya Turkana kupiga jeki juhudi za kuhimarisha viwango vya elimu kaunti hiyo badala ya kungoja msaada wa serikali kuu.
Hata hivyo amewataka vijana kaunti ya Turkana kujiunga na vyuo vya kiufundi ili waweze kujifunza taalumu mbali mbali ambazo zitawasaidia kujiajiri.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts