Serikali ya kaunti ya Pokot Magharibi imepiga hatua kwenye suala la kusambaza chakula kwa watoto wa shule zilizoko maeneo ya mashinani.
Afisa katika Shirika la DWS Tawi la Pokot Magharibi Philis Wabwire amesema serikali kaunti hiyo inafaa kuweka mikakati zaidi ya kustawisha mradi huo ili kuwafaa watoto hata baada ya janga la Corona kuthibitiwa.
Aidha Wabwire ametaja umuhimu wa Siku ya Mtoto Mwafrika kwa watoto ambao wazazi wao wanapata ugumu wa kukidhi mahitaji yao ya kismingi huku akitoa changamoto kwa wazazi kujukumika kwenye masuala ya kuwapa watoto wao chakula na malezi bora kando na masuala ya afya.
Hata hivyo ameitaka Idara ya mahakama Kaunti ya Pokot Magharibi kutenga muda katika kalenda ya mipango yake ili kuhamasisha umma kuhusu sheria na haki za watoto kama njia mojwapo ya kuafikia kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Mtoto Mwafrika.