Staa wa muziki nchini Willy Paul hatimaye amedokeza kuwa uongozi wake umemuomba msamaha baada ya kuuondoa wimbo wake na Rekless uitwao Aaaih kwenye album yake ya “Songs of Solomon.”
Akiwa kwenye moja ya interview Willy Paul amesema uongozi wake umechukua hatua hiyo baada ya wimbo huo kufikisha zaidi ya watazamaji laki saba kwenye mtandao wa Youtube.
Ikumbukwe mwishoni mwa mwaka wa 2020 Willy Paul aliachia album yake iitwayo “Songs of Solomon” iliyokuwa na jumla ya ngoma 9, Lakini baadae msanii huyo alijitokeza na kuusuta vikali uongozi wake kwa hatua ya kuufuta wimbo wa kumi kwenye album hiyo ambao alikuwa amemshirikisha msanii Rekless bila ridhaa yake.
Uongozi wa Willy Paul ulidai kuwa hawakutaka msanii huyo afanye collabo na wasanii wa muziki wa Gengetone kwani wangeharibu brand yake.