Nyota wa muziki nchini Willy Paul amefanikiwa kufikisha zaidi ya subscribers laki 6 kwenye mtandao wa youtube.
Willy Paul ambaye anafanya vizuri na mkwaju wake wa “Liar” hakuficha furaha yake ya kuwa na wafuasi wengi kwenye mtandao huo kwani ametumia ukurasa wake wa instagram kuwapa mashavu mashabiki wake kwa kumpa support kwenye shughuli zake za kimuziki ikizingatiwa kuwa sio jambo rahisi Kushawishi Watu kumfuatilia Kwenye Youtube.
Kwa mafanikio hayo, Willy Paul anakuwa msanii wa tatu nchini kuwa na subscribers wengi zaidi YouTube baada ya Otile Brown aliye na subscribers laki 6.6 pamoja na Sauti sol ambao wana subscribers laki 7.