Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania maarufu kama whozu ametangaza kuja na EP yake ya nyimbo 5.
Whozu kupitia akaunti yake ya Instagram alitangaza ujio huo wa EP yake alipokuwa siku ya kusherehekea tarehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, ‘Machi 10’ mwaka wa 2021.
Katika taarifa hiyo, Whozu hakubainisha jina na tarehe ya ujio project hiyo ambapo alieleza kuwa EP hiyo itabeba nyimbo ambazo atahakikisha zinafanye vizuri sokoni.