WAZAZI MLIMA ELGON WAMETAKIWA KUSHIRIKIANA NA IDARA ZA SERIKALI KUFANIKISHA MPANGO WA WANAFUNZI KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA KWA ASILIMIA MIA

Wazazi kutoka Chesikaki eneo bunge la Mlima Elgon wamehimizwa kushirikiana kikamilifu na vitengo mbalimbali vya serikali ili kufanikisha mpango wa asilimia mia moja ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kitaifa KCPE kujiunga na kidato cha kwanza.

Hayo ni kwa mujibu wa  chifu wa Kata ya Chesikaki Mono Ndiema ambaye amewataka wazazi kuhakikisha kuwa wanao wanafika shuleni ili wapate elimu itakayowafaidi pakubwa maishani kwani ni wajibu wa wakuu wa shule kuwaruhusu wanafunzi kusajiliwa katika kidato cha kwanza wakati wazazi wanashughulikia swala la karo.

Aidha amewataka wakaazi wa eneo hilo kushirikiana na afisi za serikali ili kufanikisha miradi mbalimbali ya serikali ikiwemo kilimo na elimu kwa watoto.

Kwa upande wake Mwakilishi wadi wa Chesikaki Ben Kipkut amepuzilia mbali madai ambayo yamekuwa yakienezwa na baadhi ya wakaazi wa eneo hilo kuwa hatamu ya uongozi wa mwakilishi wadi ni miaka kumi pekee.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts