Wawakilishi wadi katika bunge la kaunti ya Trans-Nzoia wamepuuzilia mbali madai kwamba ruzuku ya shilingi milioni nne nukta tano ya magari kwa wabunge wa kaunti kote nchini imetumika kuwahonga ili kuunga mkono ripoti ya maridhiano BBI.
Kulingana na mwakilishi wadi mteule katika bunge hilo Philip Nyongesa amesema kilichofanyika tu ni kubadilisha mikopo ya kununua magari kuwa ruzuku ambayo imekuwa katika makadirio ya kifedha ya mwaka iliyotangulia.
Kwa upande wake mwakilishi wa wadi yaSaboti David Kapoloman amewataka wabunge wa kitaifa kukoma kuingilia mabunge ya kaunti na badala yake waendelee kutekeleza majukumu yao.