WATOTO SITA WOTE WA FAMILIA MOJA SASA WATAKA USAIDIZI KUTOKA KWA IDARA YA WATOTO JIMBO LA POKOT MAGHARIBI

Familia moja ya Watoto Sita kutoka Mji wa Makutano eneo Bunge la Kapenguria kaunti ya Pokot Magharibi sasa inataka Idara ya Watoto kuingilia kati na kuwasaidia.

Watoto hao wamekuwa wakizozana na Baba yao kuhusiana na mahitaji ya kimsingi ikiwemo Chakula ambayo wanadai wanakosa.

Wakiongozwa na Philemon Rutto ambaye ndiye mtoto mkubwa katika familia hiyo, wamedai kuwa tangu kutengana na Mama yao, Baba yao amedinda kutekeleza majukumu yake kama Mzazi hali wanayosema imeathiri pakubwa Maisha yao ya kawaida.

Ruto amesema amelazimika kusitisha Masomo yake ili kushughulikia wadogo wake akisema hamna hatua ambayo imechukuliwa dhidi ya Baba yao licha ya kuwasilisha malalamishi katika Idara ya Watoto, kutokana na kuwa anafahamikiana na watu wenye uwezo.

Hata hivyo ni madai ambayo yamepuuziliwa mbali na Felix ambaye ni Baba yao anayesema ametekeleza majukumu yake kikamilifu kama Mzazi ila Watoto hao wameshawishiwa na Mama yao kuibua madai hayo dhidi yake, kauli inayoungwa mkono na baadhi ya majirani.

Alex Toilem

Alex Toilem is a kiswahili news anchor, news editor at Northrift Radio 104.9 and 104.5 fm He is also

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts