Wanasiasa wamehimizwa kusitisha cheche za matusi kwenye majukwaa ya mikutano ya hadhara na mazishini ili kupunguza joto la kisiasa ambalo linaendelea kupanda kila kuchao.
Akihutubu wakati wa mazishi kwenye eneo la Marambach Kitalale, Afisa Mkuu Mtendaji katika Wizara ya Maji, Mazingira na Maliasili katika kaunti ya Trans nzoia, John Meng’wa amesema Kenya inaweza kustawi kiuchumi na kimaendeleo iwapo viongozi wataendelea kuhubiri umoja na utangamano.
Meng’wa amewashauri viongozi kusitisha siasa mazishini na badala yake kuifariji na kuipa familia iliyofiwa muda mwafaka wa kuomboleza.