WANABODABODA TURKANA WAPOKEA PIKIPIKI

WANABODABODA TURKANA WAPOKEA PIKIPIKI

Wahudumu wa bodaboda katika kaunti ndogo ya Turkana ya kati wamefaidi na zaidi ya pikipiki kumi ambazo naibu wa rais Dakta William Ruto aliahidi kuzitoa wikiendi iliyopita kwenye sherehe ya tamaduni jamii ya turkana maarufu kama Tobong’u lore.
Akizungumza kwenye hafla ya kuwapokeza wahudumu wa bodaboda pikipiki hizo mjini lodwar, mwakilishi wa wadi ya Lodwar township Robert Lowoko amesema pikipiki hizo zitapokezwa kila kundi la wanabodaboda ambalo limejiandikisha kama chama cha ushirika na wala sio mtu binafsi.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa wana bodaboda katika kaunti ya Turkana Peter Namwii amepongeza hatua ya naibu wa rais Dakta William Ruto kuwapa vijana pikipiki hizo ambazo amesema zitawasaidia kujikwamua kiuchumi na kimaisha.
Hata hivyo mwakilishi wa wadi ya lodwar towship Robert  Lowoko ametumia fursa hiyo kuwarai vijana kaunti ya turkana kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye zoezi la sensa ambalo litaanza tarehe  24 mwezi huu wa  Agosti.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts