Wakulima wadogo wadogo nchini wananuia kupanua mauzo yao kwenda kwa soko la Uchina ili kupata faida zaidi.
Mkurugenzi mkuu wa muungano wa wakulima wadogo wadogo Justus Lavi Mwololo anasema kuwa masoko ambayo Kenya hupeleka bidhaa zake kama vile Marekani na Ulaya,yanakabiliwa na changamoto kutokana na vizuizi vya kibiashara vilivyowekwa ili kudhibiti msambao wa virusi vya COVID-19.
Kulingana na Mwololo ,China imeweza kukabiliana na janga la COVID-19 huku ikifungua tena soko lake kwa uagizaji wa bidhaa kutoka nje na hivyo ni fursa nzuri kwa wakulima wa maembe, parachichi na bidhaa nyingine za kilimo.
Mwololo ameongeza kuwa taifa hilo la Afrika Mashariki limekuwa likiuza kiasi kidogo tu cha mazao yake ya kilimo nchini China lakini sasa wakulima wadogo wanapanga kuongeza.