Wito umetolewa kwa serikali ya kaunti ya bungoma kuwatafutia wakulima wa zao la kahawa leseni itakayowawezesha kuuza zao hilo kwa bei nafuu ili kuinua pato lao.
Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha Kimabole eneo Bunge la Mlima Elgon Robert Sikulu anahoji kuwa iwapo serikali ya kaunti hiyo itawapa leseni ya kuuza zao hilo, wakulima wataweza kunufaika pakubwa na kilimo hicho ikilinganishwa na sasa ambapo bei yake ni duni
Aidha Sikulu amewalaumu wauzaji zao hilo kwa kile anachodai kukawia kuuza kahawa hali ambayo inachangia kushuka ubora wake.